• By Humphrey Makussa

DC AENDELEA NA UKAGUZI SHULE ZA MSINGI KIBAHA

Updated: Jan 25

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mheshimiwa Martin Ntemo ambaye yuko katika ziara ya kukagua mapokezi ya wanafunzi wanaoanza kidato cha nne na darasa la kwanza, amebainisha kuwa nguvu za wananchi pamoja na halmashauri hazina budi kuongezwa ili kuhimili ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiandikisha mashuleni kwa sasa.


‘Nimeona jitihada zinazofanyika katika baadhi ya shule lakini bado tuna haja ya kuongeza nguvu zaidi, idadi ya wanafunzi ni kubwa na itaendelea kuongezeka kataka miaka ijayo pia’ alisisitiza DC Ntemo.


Aidha, Mhe. Mkuu wa wilaya alisema pamoja na ongezeko la wanafunzi mashuleni bado hali ya madarasa inahitaji maboresho. Madarasa mengi yamebomoka sakafu na samani hasa za mbao zimeharibika sana kama vile madawati, madirisha na milango, vyote vinahitaji kuboreshwa.


Mpango wa Elimisha Kibaha Awamu ya Pili unatarajiwa kuanza hivi karibuni ili kuhakikisha kuwa wadau wengi zaidi wanashirikishwa katika shughuli za maendeleo wilayani Kibaha na hususan zinazo husiana na elimu. Mpango wa Elimisha Kibaha kwa mwaka jana ulichangia ujenzi wa vyumba vya madarasa 31 ambavyo vimekuwa ni msaaada mkubwa katika kupokea ongezeko hili la wanafunzi linaloshuhudiwa wilayani humo.


Wilaya ya Kibaha ni moja ya wilaya ambazo zimekuwa zikifanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba na kidato cha nne.Zifuatazo ni picha za DC alipotembelea shule za Kilangalanga, Azimio na Mtongani zilizopo Mlandizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini.


14 views
RECENT POST