• raymhtz2

DC NTEMO AZINDUA CHANJO YA UVIKO 19 MAFIA

Mkuu wa Wilaya ya Mafia Eng. Martin Ntemo amezindua utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 (COVID 19) katika wilaya ya Mafia siku ya Jumatatu ya tarehe 9 Agosti, 2021.

Mara baada ya kupata chanjo hiyo, Eng. Ntemo aliwahamasisha wananchi kujitokeza kwa kuelezea kuwa, mbali na faida zake kama kinga, lakini pia inapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vinavyotokana na ungonjwa huo. Aidha, ameelezea kuwa chanjo hiyo husaidia kupunguza makali ya homa ya ugonjwa huo kwa muathirika.

Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa tayari dozi 1,000 zimepokelewa wilayani Mafia na kwamba kwa awamu hii ya kwanza zitaanza kutolewa kwa wauguzi na watoa huduma za afya wilayani humo, watumishi wa umma, wahudumu katika mahoteli na migahawa, wazee na watu wenye umri wa zaidi ya miaka 45 ambao pia wana changamoto ya maradhi ya muda mrefu.

Vituo vya kutolea chanjo hiyo vimeelezwa kuwa ni katika Hospitali ya Wilaya (Mafia) na katika zahanati za; Kirongwe, Bweni, Baleni, Chemchem na Utende.


DC Eng. Martin Ntemo akipewa chanjo ya UVIKO 19 na mhudumu wa huduma za afya kuzindua kampeni ya huduma hiyo wilayani Mafia.10 views
RECENT POST