• By Humphrey Makussa

LEO AGOSTI 18 MKUU WA WILAYA YA MAFIA AKABIDHI MWENGE KWA MKUU WA MKOA WA PWANI

Mkuu wa wilaya ya Mafia, Mhandisi Martin Ntemo, leo Agosti 18, 2021 amekabidhi Mwenge maalum kwa wa Uhuru kwa mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhe. Aboubakari Kunebge katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julias Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam ukitokea visiwani Mafia ambapo umeweza kutembelea jumla ya miradi 9 yamaendeleo.


Mwenge huo unatarajiwa kuwa jijini Dar es Salaam kwa siku tano ambazo utapitia miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya Shillingi Billion 105.1. Leo tarehe 18 Agosti utaanzia mbio zake katika Jiji la Ilala kisha katika Wilaya za Ubungo, Kinondoni, Kigamboni na Temeke ambapo ifikapo August 23 Mwenge huo utakabidhiwa kwa Mkoa wa Lindi ukienda na kaulimbiu inayolenga kuhimiza Matumizi sahihi ya TEHAMA.


Mkuu wa wilaya ya Mafia, Mhandisi Martin Ntemo (kulia) akikabidhi Mwenge kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakari Kunenge.

5 views
RECENT POST