• raymhtz2

UZINDUZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA CHANJO ZA MIFUGO NEEMA KWA WAFUGAJI NCHINI


Waziri wa Mifugo na uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki amefanya zira ya kikazi kukagua ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza chanjo za mifugo kiitwacho Hester Biosciences Africa Limited, kinachojengwa mjini Kibaha mkoani Pwani. Katika ziara hiyo Waziri wa Mifugo na Uvuvi aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Eng. Martin Ntemo. Ziara hiyo ameifanya ndani ya wiki chache tangu kuapishwa kushika nafasi hiyo baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


“Uwepo wa Kiwanda kikubwa cha kutengeneza chanjo mbalimbali za mifugo hapa nchini ni neema kwa wafugaji wetu, kwani mbali na kupata chanjo za mifugo yao kwa uwepesi na bei nafuu, watapata pia elimu ya namna ya ufugaji bora ili kupata mavuno bora na yenye tija kwao na hatimaye Taifa kwa ujumla” Waziri Ndaki aliyasema hayo baada ya kupokea taarifa fupi toka kwa msimamizi wa mradi (Project Co-ordinator) Bi. Tina Towo Sokoine.

Pichani, Mh. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Mashauri Ndaki akisalimiana na wawekezaji wa kiwanda cha Hester, na pembeni yake ameambatana na Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kibaha

Eng. Martin Ntemo.

Mh. Waziri (menye shati la blue bahari) akiwa na mwenyeji wake Mh. Mkuu wa wilaya ya kibaha (wa pili kutoka kushoto) wakipata maelezo ya mpangilio wa kiwanda cha Hester katika

ramani picha (model plan).

Picha ya pamoja ya Mh. Ndaki na mwenyeji wake mkuu wa wilaya Eng. Martin Ntemo pamoja na msimamizi wa mradi (Project Co-ordinator) Bi. Tina S. Sokoine. Wengine waliokaa kulia ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Nd. Mussa Abdallah Ndomba, na anayefuatia ni Rajiv Andhi Mkurugenzi wa Hester (CEO & Managing Director)

5 views
RECENT POST