• raymhtz2

MACHINJIO YA KISASA KIBAHA KUCHINJA MBUZI 4,000 NA NGOMBE 1,000 KWA SIKU


Sekta ya vianda nchini Tanzania imezidi kukua na kuandika historia mpya katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki, kwa kushuhudia wawekezaji wakikamilisha ujenzi wa machinjio kubwa na ya kisasa iliyojengwa maeneo ya Soga wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.


Wakisoma ripoti yao mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki, wawekezaji hao walisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 50, unatarajia kutoa ajira za moja kwa moja zisizopungua 500, na wanatarajia kuchinja mbuzi hadi 4,000 na ngombe 1,000 kwa siku kama kiwanda kitafanya uzalishaji kwa kiwango chake cha juu.


Aidha, Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Mh. Eng. Martin Ntemo amewashauri wawekezaji hao katika kutoa kipaumbele cha ajira kwa vijana wengi ambao ni wakazi wa eneo hilo la Soga na maeneo ya jirani, haswa vijana waliopitia mafunzo ya jeshi la Akiba katika swala zima la ulinzi.

5 views
RECENT POST