• By Humphrey Makussa

MAONESHO YA TANTRADE YAFANYIKA DAR

Maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yaliyoandaliwa na TANTRADE yamefanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 3 Desemba, 2020 hadi 09 Desemba, 2020. Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Eng. Martin Ntemo alikuwa ni mmoja ya watu waliotembelea katika maonesho hayo na kujionea bidhaa mbali mbali zinazozalishwa na wajasiliamali hapa nchini.


Eng. Martin Ntemo alitumia fursa hiyo kuipongeza TANTRADE kwa maandalizi hayo na kutoa rai kuwa kwa siku zijazo ijitahidi kutoa matangazo ya kutosha ili kuhamasisha ushiriki Zaidi. Aidha, wajasiliamali pia wamepongezwa kwa namna wanavyoendelea kuboresha bidhaa zao ikiwa ni pamoja na kuzalisha vifungashio ambavyo vina viwango na muonekano mzuri.


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Eng. Martin Ntemo akipata maelezo katika banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipotembelea kujionea maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania.


Mhe. Eng. Martin Ntemo akisaini katika kitabu cha wageni kwenye ofisi za TANTRADE zilizoko ndani ya viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaa, alipotembelea kujionea maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania.


Mhe. Akipata maelezo kuhusu bidhaa zinazozalishwa na wajisiliamali


5 views
RECENT POST