• By Humphrey Makussa

MKURUGENZI WA MJI KIBAHA ATOA ONYO UNUNUZI WA ARDHI KIHOLELA


Mkurugenzi wa mji Kibaha Bi. Jenifa Omolo ameonya tabia ya kununua ardhi bila kufuata taratibu na bila kujiridhisha kuhusu uhalali wa eneo husika kabla ya kufanya malipo yoyote.


Bi. Jenifa ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mgogoro wa ardhi ambao umedumu kwa muda mrefu baina ya makundi mbali mbali ya watu waliovamia shamba la mwekezaji katika eneo la Zegeleni Kata ya Visiga wilayani Kibaha.


Mkurugenzi huyo alikuwa katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Martin Ntemo alipotembelea eneo hilo ili kutatua mgogoro wa ardhi ambao ulifikia hatua ya kuashiria kutokea kwa uvunjifu wa amani.


Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa Sheria ya Ardhi No. 82 inamnyang’anya Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wake mamlaka ya ardhi. ‘Lazima niwape elimu ili msiendelee kuibiwa na kuingia katika migogoro ya ardhi kwani ardhi yote iliyopo mijini mwenye mamlaka ni Mkurugenzi wa Halmashauri na si vinginevyo’ alifafanua Zaidi.


Akinukuu maelekezo ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi, Mkurugenzi aliwaasa wananchi hao “Ndugu wananchi, kabla hamjanunua ardhi maeneo ya mijini nendeni ofisi za ardhi za wilaya mkathibitishe kama hayo maeneo ni halali na hapa Wenyeviti wa Mitaa hamtakiwi kujihusisha na uuzaji wa ardhi, mtafungwa”.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Bi. Jenifa Omolo akifafanua kuhusu sheria taratibu, haki na wajibu wa wanakijiji kuhusu maswala ya ardhi.


Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Martin Ntemo akisisitiza kuwepo kwa maelewano chanya baina ya wakazi wa Zegereni na viongozi wa serikali ya mtaa ili kuleta amani na kuepuka

migogoro isiyo ya lazima.

Wakazi na wanunuzi wa ardhi katika eneo la Zegereni wakisikiliza kwa makini elimu, ushauri na maelekezo toka kwa Mkuu wa wilaya na jopo la viongozi wa halmashauri ya mji Kibaha alioongozana nao.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Zegereni akitoa maelezo kuhusu historia ya mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka kadhaa kijijini hao.

Mh. Diwani wa eneo hilo la Zegereni akifafanua jambo kuhusu mgogoro huo wa ardhi.

9 views
RECENT POST