• By Humphrey Makussa

UONGOZI CHAMA CHA SKAUTI WILAYA YA KIBAHA WAMTEMBELEA MKUU WA WILAYA

Uongozi wa Chama cha Skauti kutoka wilaya ya Kibaha umefanya ziara ya utambulisho kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Martin Ntemo. Ujumbe huo uliojumuisha wajumbe 6 uliongozwa na; Bi. Azama Hassan ambaye ni Kamishna wa Chama cha Skauti kwa wilaya ya Kibaha, Bw. Halfani Omari (Mratibu wa Programu za Vijana – Kibaha), Bi. Samaha Ramadhani Kitogo (mwakilishi kutoka Kilangalanga), Bw. Salum Awadh (mwakilishi kutoka Kilangalanga), Bw. Erick Ngimba (Kamishna Msaidizi – Kibaha Vijiini) na Bw. Baraka Maluila (Kamishna Msaidizi – Kibaha Mji.)


Ziara hiyo ya ujumbe wa skauti pia ili ambatana na hafla fupi ya kumvisha skafu mkuu wa wilaya ya Kihaba ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi kuwa mlezi wa chama cha skauti kwa wilaya ya Kibaha.


Chama cha skauti kinajihusisha na ulezi wa vijana ili kuwafundisha kuwa wazalendo, wakakamavu na wenye maadili mema, kikilenga nchi yetu kupata Taifa bora lenye viongozi wazalendo wenye kuipenda nchi yao.


Mkuu wa wilaya akiwa na ujumbe wa Chama cha Skauti walipomtembelea ofisini kwake.


Bi. Samaha Kitogo akimvisha skafu mkuu wa wilaya.

Kamishna wa Chama cha Skauti wilaya ya Kibaha Bi. Azama Hassan akikabidhi taarifa ya chama hicho kwa mkuu wa wilaya ya Kibaha.

11 views
RECENT POST