• raymhtz2

VIKUNDI VYA FAIDIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI MAFIA

Vikundi mbalimbali katika jamii vyaendelea kufaidika na mikopo itolewayo na Halmashauri ya Mafia katika kuwawezesha wananchi kiuchumi. Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya Mhandisi Martin Ntemo akiwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Hassan Pango na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya walitembelea vikundi hivyo na kuongea na wafaidika hao ili kujua maendeleo yao na namna mikopo hiyo ilivyowasaidia kiuchumi na kijamii pia.


Mkuu wa Wilaya Eng. Martin Ntemo akiwa na Mwenyekiti wa CCM(W) Ndugu Hassan Pango(mwenye kofia nyeusi) na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya, wakiongea na moja ya kikundi cha wakina-mama ambao wamefanikiwa na mikopo ya Halmashauri.Lakini pia walipata fursa ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo

wilayani Mafia.

1 view
RECENT POST